Lulu akiingia mahakamani leo. |
Mama mzazi wa Lulu, wa pili kutoka Kushoto akiwa Mahakamani leo |
Lulu akicheka kwa aibu baada ya kushawishiwa na mwandishi mmoja wa kike ampige picha |
Lulu akiwa mahakamani kusikiliza Hatma ya dhamana yake na masharti |
Mahakama kuu leo imetangaza
dhamana ya mwigizaji Lulu iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni
pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam,
kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja
na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za
kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema
masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu
la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha
ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba
uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa
sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio
walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.
Picha zote na MillardAyo.Com